MBALI na benchi la ufundi la Yanga kuwa na mabadiliko kwenye mchezo wa jana, Uwanja wa Mkapa pia kwenye upande wa wachezaji kulikuwa na mabadiliko makubwa tofauti na awali.
Kwa sasa Yanga ipo chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ambaye alichukua mikoba ya Cedric Kaze aliyechimbishwa na katika mchezo wa kwanza wakati ubao ulisoma Yanga 1-1 Simba yeye alikuwa kwenye benchi la ufundi.
Kwenye kikosi chake alianza na :-Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe,Tuisila Kisinda, Feisal Salum, Michael Sarpong , Ditram Nchimbi , Farid Mussa.
Katika kikosi cha jana kulikuwa na mabadiliko ya wachezaji 6 ambao walianza kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ambao ni pamoja na Metacha Mnata ambaye alisimamishwa mechi tatu kutokana na tatizo la nidhamu, pamoja na Lamine ambaye naye ni tatizo la nidhamu Mustapha anatibu majeraha ya nyama za paja, Sarpong kwa mujibu wa ripoti ni kwamba anaumwa huku Farid Mussa na Ditram Nchimbi wakianzia benchi.
Wapya ambao walianza ilikuwa ni Farouk Shikalo Dickson Job, Zawad Mauya, Adeyum Saleh,Deus Kaseke na Yacouba Songne.
Kikosi kamili cha Yanga kilikuwa namna hii: Farouk Shikalo, Kibwana, Adeyum, Job, Mwamnyento, Mukoko, Mauya, Tuisila,Kaseke.Feisal na Yacouba.
Kwa upande wa Simba ni benchi la ufundi ambalo limefanyiwa mabadiliko ni Sven Vandenbroeck alikuwa kwenye benchi la ufundi jana mikoba yake ilikuwa mikononi mwa Didier Gomes.
Novemba 7 kikosi kilikuwa namna hii:- Aishi Manula, Kapombe Shomari,Mohamed Hussein, Joash Onyango, Pascal Wawa, Rally Bwalya, Mzamiru Yassin, John Bocco, Clatous Chama na Luis Miquissone.
Chini ya Gomes mabadiliko katika kikosi cha kwanza aliyekosekana alikuwa ni Jonas Mkude, Rarry Bwalya aliyeanzia benchi na Mzamiru Yassin na ingizo jipya katika kikosi cha kwanza mbele ya Gomes ilikuwa ni Bernard Morrison na Erasto Nyoni.
Kikosi cha Simba kilikuwa namna hii:Manula, Kapombe,Hussein, Onyango, Wawa, Lwanga,Morrison,Nyoni, Bocco, Chama na Miquissone.
Mchezo huo baada ya dk 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga.