news

COASTAL UNION YAIVUTIA KASI SIMBA

admin July 5, 2021 10:47 am


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa maandalizi ya timu yake kuelekea mechi zilizobaki yapo vizuri na wanaamini watapata matokeo chanya.


Mchezo ujao wa Coastal Union inayopambana kujinasua kutoka hatari ya kushuka daraja ni dhidi ya Simba  unatarajiwa kuchezwa Julai 19, Uwanja wa Mkapa.

Mgunda amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi hivyo anaamini kwamba vijana wake watafanya vizuri.

“Vijana wapo vizuri kwani kila mchezaji anajua kwamba tunahitaji ushindi na mechi zetu ambazo zimebaki ni lazima tupambane hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti.

“Kila mmoja anahitaji kuona kwamba tunarejesha hali ya kujiamini na hilo linawezekana hasa ukizingatia kwamba kila timu inahitaji kupata pointi tatu,” amesema Mgunda.

Mchezo wao uliopita walipokutana, Mgunda alishuhudia ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ukisoma Coastal Union 0-7 Simba na hat trick ya kwanza ya John Bocco ilikusanywa hapo.

VIDEO: YANGA KUENDELEZA UBABE KIGOMA, SIMBA WALIA NA MZEE MPILI POLISI TANZANIA YATAKA TANO BORA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply