Ligi Kuu

POLISI TANZANIA YATAKA TANO BORA

admin July 5, 2021 10:47 am


 UONGOZI wa Polisi Tanzania umeweka wazi kwamba utapambana kufikia malengo waliyojiweka kumalizi ligi ndani ya tano bora.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 42 kwenye msimamo ipo nafasi ya 7 nafasi ya tano ipo kwa Namungo FC yenye pointi 43.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa kila mmoja ana mipango ya kufanya vizuri hivyo nao pia wanahitaji kutimiza malengo yao.

“Malengo yetu ni kuona kwamba timu inamaliza ndani ya tano bora kwani kila mchezaji anapenda kuona timu inashinda hasa kwa mechi ambazo zimebaki.

“Kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani wamekuwa wakifanya hivyo kwenye mechi ambazo tumekuwa tukicheza hilo ni faraja kwetu na kila kitu kinawezekana,” amesema.

Mchezo wao ujao wa ligi ni dhidi ya Kagera Sugar ambapo unatarajiwa kuchezwa Julai 14, Uwanja wa Ushirika, Moshi. 

COASTAL UNION YAIVUTIA KASI SIMBA KOCHA GOMES YUPO TAYARI KUWAJIBISHWA KWA KUPOTEZA MBELE YA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply