Baada ya kupoteza mchezo wa jumamosi dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu Didier Gomes amesema matokeo hayo yametuumiza kwani tumewaangusha mashabiki wetu ambao walikuwa na matumaini makubwa.
Gomes amesema tulipaswa kushinda kwenye mchezo mkubwa na kutawazwa mabingwa wa ligi lakini haikutokea hivyo yeye kama kocha mkuu anapaswa kubeba jukumu hilo.
Raia huyo wa Ufaransa amesema hatukucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza na tulipoteza pasi na kuruhusu kushambuliwa zaidi kitu ambacho hatukutarajia kutokea.
โNi matokeo ambayo hatukuyategemea yametuumiza na tumewaangusha mashabiki wetu. Tulistahili kushinda kwenye mechi kubwa ili kutawazwa mabingwa lakini haikutokea.
โHatukucheza vizuri kipindi cha kwanza lakini cha pili tulikuwa bora na tulitengeneza nafasi za kufunga lakini hatukuwa na bahati,โ amesema Gomes.