kimataifa

RAMOS: NINAFURAHI KUWA PSG

admin July 9, 2021 5:47 am


SERGIO Ramos nyota mpya wa PSG amesema kuwa hatasau tukio hilo katika maisha yake baada ya kusaini dili la miaka miwili bure baada ya mkataba wake kuisha ndani ya Real Madrid.

Nyota huyo ameongeza kuwa anafurahi kuwa ndani ya PSG jambo ambalo anaamini kwake litakuwa na matokeo chanya.

Nyota huyo mwenye miaka 35 ameibukia hapo akitokea kikosi cha Real Madrid ambapo alidumu huko kwa muda wa miaka 16 na mabosi wa timu yake hiyo ya zamani waligoma kumuongezea dili refu la miaka miwili ambayo alikuwa akihitaji ili abaki ndani ya kikosi hicho.

Akiwa ndani ya Real Madrid, aliweza kushunda jumla ya mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mataji matano ya La Liga na mataji manne ya Kombe la Dunia kwa Klabu. 

 Anaungana na nyota wengine ambao ni pamoja na  Achraf Hakimi na Georginio Wijnaldum ambao wameshasaini ndani ya PSG iliyo kwenye mpango wa kukamilisha dili la Gianluigi Donnarumma.

Ramos amesema:”Ninafuraha kubwa kujiunga na Paris Saint-Germain. Hii ni nafasi kubwa kwangu na ni siku ambayo sitaisahu kabisa,”.



VIDEO: YANGA: TUNAKWENDA KIGOMA KUPIGA PALEPALE KWENYE MSHONO VIDEO: YANGA WAFURAHIA DILI LA AZAM TV

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply