WABABE Italia na England wanatarajiwa kukutana Uwanja wa Wembley mbele ya mashabiki 60,000 ambao wameruhusiwa kushuhudia live fainali ya Euro 2020.
Inakuwa ni fainali ya 16 katika michuano ya Euro ambapo ilipaswa kufanyika mwaka jana ila ilighairishwa kutokana na janga la Corona na ilianza kutimua vumbi Juni 11,mwaka huu.
Italia ilikuwa miongoni mwa timu 24 ambazo zilishiriki michuano hii ambazo zilicheza kupitia viwanja vya nchi 11 na ilitinga hatua ya fainali baada ya kuwaondoa Hispania kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya muda wa kawaida kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1.
England ilitinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Denmark na imefungwa bao moja tu katika hatua ya nusu fainali ikiwa ni mara ya kwanza kutinga hatua ya fainali.