NYOTA wa Azam FC ambaye ni namba moja kwa kucheka na nyavu kwa msimu wa 2020/21 alikuwa ni mwiba kwa makipa ambapo aliweza kuwatungua kila alipopata nafasi ya kuanza.
Ni Prince Dube, huyu ni muuaji anayetabasamu kwa kuwa akifunga lazima aache tabasamu ila majeraha yamekuwa yakiyeyusha ndoto zake kwa kuwa ni namba moja kwa Azam FC akiwa na mabao 14.
Timu yake imemaliza ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi na imefunga jumla ya mabao 50 ambapo yeye amehusika kwenye mabao 19 akiwa ametengeneza nafasi tano za mabao.
Kasi yake ilikuwa namna hii:-Bao moja mbele ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Azam Complex, mabao mawili mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Azam Complex, bao moja mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela, mabao mawili mbele ya Kagera Sugar.
Uwanja wa Azam Complex, bao moja mbele ya Mwadui FC, Uwanja wa Azam Complex, bao moja mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Azam Complex, bao moja mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.
Mabao mawili mbele ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Azam Complex, moja alifunga kwa penalti,bao moja mbele ya KMC, Uwanja wa Azam Complex, bao moja mbele ya Yanga, Uwanja wa Mkapa,bao moja mbele ya Namungo FC, Uwanja wa Azam Complex.