Azam FC

BAADA YA KUMALIZANA NA MANARA..HANS POPE ‘AWAFOKEA’ YANGA

admin July 30, 2021 3:00 am


Mmoja ya vigogo wa Simba, Zacharia Hanspope amesema ubora wa kikosi cha Simba ndio sababu ya kupata mafanikio makubwa msimu huu, huku akiahidi kuendelea kuwaburuza watani zao, Yanga kwa kubeba makombe zaidi msimu ujao ikiwemo ubingwa Afrika.

Hanspoppe alisema Yanga hawawawezi hata kidogo na wala si levo yao na ndio maana hata walipochukua ubingwa wa Mapinduzi wala haukuwaumiza kwani ni kama kombe la kufanyia mazoezi upande wao.

Kigogo huyo ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ambaye aliwasili jana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pamoja na kikosi cha Yanga ikiwa ni saa moja tu tangu Simba wawasili kwa ndege nyingine wakitokea Kigoma timu hizo zilikocheza fainali ya ASFC juzi na Wekundu wa Msimbazi kutwaa ubingwa.

“Simba inatisha sana na ukiona kuna timu ilitufunga ujue ilibahatisha kwani hata mechi ya ligi ambayo Yanga ilishinda bao 1-0 walibahatisha tu kwa sababu hawakutufunga, ila tulijifunga maana mpira ulimgonga mchezaji wetu ukaingia golini hivyo wasijisifu,” alisema.

WAKATI MSUVA AKING’ARA..CHILUNDA MAMBO YAMWENDEA KOMBO MOROCCO GOMES ALIANZISHA MSIMBAZI..AWEKA WAZI MSIMAMO WAKE KWA MSIMU UJAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply