Simba SC

MO AKABIDHI HUNDI YA BILIONI 20, MCHAKATO WA MABADILIKO UMEKAMILIKA

admin July 30, 2021 10:43 am


 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji,’Mo’ leo Julai 30 amekabidhi mfano wa hudni yenye thamani ya Bilioni 20.

Mkwanja huo ni kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa mabadiliko ndani ya Simba ambao unaendelea na ulikuwa kwenye hatua za mwisho za kuukamilisha mchakato huo.

Mo ameweka wazi kuwa amekuwa akishirikiana na viongozi wa Simba pamoja na mashabiki katika kutafuta mafanikio ambapo timu hiyo imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo na imetwaa Kombe la Shirikisho mara mbili.

Mbele ya Waandishi wa Habari Mo amesema:-“Leo naweka hiyo Bilioni 20 ya hisa asilimia 49 mbele ya mdhamini wa klabu na mwenyekiti wa klabu.

Pia ameweka wazi kwamba mchakato wa mabadiliko umekamilika baada ya kupata hati kutoka FCC ya kuruhusu kumalizia mchakato.

MAYELE ATAJA SIKU YA KUJA KUSAINI YANGA UKIACHANA NA BARBARA, HIZI HAPA SABABU NYINGINE ZA MANARA ‘KUFYEKWA’ MSIMBAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply