Home Azam FC AZAM FC BADO WAPO IMARA

AZAM FC BADO WAPO IMARA


 KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati amesema kuwa bado wana imani ya kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara ili kuweza kupata pointi tatu.

Kwenye msimamo baada ya kucheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 64 na kinara ni Simba mwenye pointi 73.

Mchezo wao uliopita kwenye ligi walilazimisha sare ya bila kufungana na Namungo FC, pia ilipoteza nafasi ya kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Simba.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa Uwanja wa Majimaji, Songea na alikuwa ni Luis Miquissone aliyepachika bao la ushindi kwa pasi ya Bernard Morrison aliyeanzisha faulo harakaharaka.

Bahati amesema:”Bado mapambano yanaendelea na kila mchezaji anajua kwamba mechi zilizobaki tunahitaji ushindi hivyo kikubwa ni kuona kwamba tunashinda.

“Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kila mchezaji anajua kwamba ni kitu gani ambacho tunahitaji, muhimu kufanya vizuri,” amesema. 


SOMA NA HII  BAADA YA KUKIWASHA VILIVYO MTIBWA....NDEMLA KURUDI MJINI KIULAINII...DOMAYO, MBOMBO KUMPISHA AZAM....