Home news RASMI: SAMATTA ASAINI MIAKA MITATU FENERBANCE

RASMI: SAMATTA ASAINI MIAKA MITATU FENERBANCEDEAL done, Mtanzania Mbwana Samatta amemalizana na klabu ya  FenerbahΓ§e ya Uturuki, amesaini mkataba wa miaka mitatu (2021-2024) baada ya kuichezea kwa mkopo kwa mwaka mmoja akitokea Aston Villa.

Samatta alijiunga na Aston Villa ya nchini England mwaka 2020, alicheza nusu msimu kisha akapelekwa kwa mkopo wa mwaka mmoja Fenerbahce ambao wameamua kumnunua moja kwa moja, ili kuwatumikia kwa miaka mitatu.

Mtandao wa Fenerbance umeweka wazi kumaliza kwa Samatta ambaye atawatumikia ndani ya miaka hiyo mitatu, baada ya kuonja huduma yake kwa mwaka mmoja.

Baba mzazi wa mchezaji huyo, ameliambia Soka la Bongo leo Jumamosi ya Juni 3, mwaka 2021 kwamba kijana wake ni mali halisi ya Fenerbahce na kwamba amevunja mkataba na Aston Villa ambao ulibakia.

“Aliondoka nchini juzi, Juni Mosi, walikaa kikao kuanzia asubuhi hadi usiku baina ya viongozi wa timu hizo mbili, kisha wakakubaliana Samatta kumnunua moja kwa moja;

Ameongeza kuwa “Nimewasiliana na Mbwana ameonyesha kufurahia jambo hilo, hivyo namuombea kheri ya kuendelea kupambana hadi atimize ndoto zake anazozitamani katika maisha yake,” amesema.

SOMA NA HII  AMKENI AMKENI...WAMEMRUDISHA TENA TSHISIMBI LIGI KUU...KAPEWA MIAKA MIWILI YA NGUVU KUKIPIGA MSIMU UJAO...