Home Simba SC BERNARD MORRISON AKABIDHIWA TUZO YA MCHEZAJI BORA

BERNARD MORRISON AKABIDHIWA TUZO YA MCHEZAJI BORA


 KIUNGO Mshambuliaji wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison, amekabidhiwa kitita cha shilingi Ml 1, kutoka kampuni ya Emirate Alluminium baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi Juni.

Nyota huyo mzee wa kuchetua ametwaa tuzo hiyo baada ya kura za mashabiki kupigwa kwa wingi kupitia mitandao ya kijamii.

Alitwaa tuzo huyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzake ambao ni Luis Miquissone na nahodha wake John Bocco, ambapo walikuwa wakiwania tuzo hiyo pamoja.

 

Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa na Kampuni ya Emirate Alluminum kila mwezi, huku mchakato wa kumpata mshindi huendeshwa na Simba kupitia kura za mashabiki wa klabu hiyo.

SOMA NA HII  MASHABIKI WA SIMBA MZUKA UMEPANDA, UNAJUA KWANININI? ISHU IKO HIVI