Home Uncategorized KMC YAONYOOSHA MABAO 2-1 KARIOBANG SHARK

KMC YAONYOOSHA MABAO 2-1 KARIOBANG SHARK


KIKOSI cha KMC leo kimeibuka kidedea kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Kariobang Sharks uliochezwa uwanja wa Uhuru.

Ofisa Habari wa KMC, Anwar Bide amesema kuwa ni mwanzo mzuri  kwao kuelekea mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Kigali utakaochezwa Agosti 10.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani ila mwisho wa siku tumeibuka na ushindi wa mabao 2-1 ni mwanzo mzuri kwetu kwa ajili ya michezo yetu ya kimataifa na tuna imani ya kufanya vizuri,” amesema.

Mabao ya KMC yamepachikwa kimiani na Serge Nogues pamoja na Vitalis Mayanga.

SOMA NA HII  NGUVU YA KIKOSI CHA KMC ZINAHAMIA HUKU KWA SASA, LEO KUANZA MITIZI YA MAANA