Home Uncategorized ISHU YA KUFUNGIWA MASHABIKI JKT TANZANIA WAOMBA MSAMAHA

ISHU YA KUFUNGIWA MASHABIKI JKT TANZANIA WAOMBA MSAMAHA


UONGOZI wa JKT Tanzania umesema kuwa makosa waliyoyafanya Juni 17 kwa kushindwa kufuata muongozo uliowekwa na Serikali kwa kushindwa kuweka umbali wa mita moja wanahitaji msamaha.

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Abdalah Mohamed,’Bares’ amesema kuwa wanahitaji msamaha wa makosa yao kwani mechi ilikuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo huo ulikuwa kati ya JKT Tanzania na Yanga na ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

“Ilikuwa ni mechi ngumu na mashabiki wengi walijitokeza kuona namna gani mchezo utakuwa ila mwisho wa siku utaratibu haukkufuatwa tunaomba radhi katika hili,” amesema.

JKT Tanzania imezuiwa kucheza na mashabiki kwa mechi zake zote zilizobaki za ushindani kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na mechi zao ambazo zimebaki ni pamoa na Mbao, Singida United na Alliance

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AWAKA VIBAYA, AZUNGUMZIWA KUFANYIWA UBAGUZI - VIDEO