Home Yanga SC HIVI NDIVYO NAMNA YANGA ITAKAVYOWAVUA UBINGWA SIMBA KUPITIA MORRISON

HIVI NDIVYO NAMNA YANGA ITAKAVYOWAVUA UBINGWA SIMBA KUPITIA MORRISON

 

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa, bado unafuatilia kesi ya winga Bernard Morrison ambaye amehamia Simba, huku wakiweka wazi kuwa wanaamini haki itatendeka, na endapo Simba watatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara basi watapokonywa kwa kuwa wamemchezesha mchezaji asiyekuwa halali.

 

Bernard Morrison kwa sasa anacheza katika Klabu ya Simba, ambapo kabla ya kujiunga na klabu hiyo alikuwa akiichezea Yanga, huku usajili wa kuhamia Simba ukigubikwa na utata mkubwa kwa madai kuwa kabla hajajiunga na Simba tayari alikuwa ana mkataba wa miaka miwili.

 

Ili watangazwe rasmi kuwa mabingwa, Simba inahitaji ushindi kwenye mchezo mmoja kati ya michezo mitano waliyobakiza hadi sasa.

 

Aidha baada ya Morrison kujiunga na Simba, Yanga waliamua kupeleka kesi hiyo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Kimichezo (Cas) inayoendelea kufanyia kazi kesi hiyo.

 

Chanzo chetu cha ndani kimeliambia Championi Jumatano kuwa: “Bado kesi ya Morrison ipo katika mamlaka husika ya usuluhishi ambapo kesi hiyo ina namba CAS 2020/A/7397 na inatarajiwa kusikilizwa kati ya Julai 18 hadi 20, mwaka huu mbele ya jaji Patrick Steward mwenye uraia wa England.


Hivyo kama Yanga watashinda kesi hiyo na Simba wakiibuka mabingwa, ni wazi kuwa watapokonywa na Yanga watakuwa mabingwa kama ambavyo imejitokeza kule nchini DR Congo ambapo AS Vita walipokonywa ubingwa na kisha kupewa TP Mazembe.

 

AS Vita pia walikuwa na matatizo ya kumtumia mchezaji ambaye hakustahili kutumiwa, ukija kwa Simba Bernard Morrison ameshacheza mechi nyingi za Simba, hivyo ikionekana wana makosa kumchezesha basi ubingwa atapewa yule aliyemaliza nafasi ya pili.

 

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa: “Msimu huu lazima tushinde makombe matatu, baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, tunakwenda kutwaa ubingwa wa Shirikisho kule Kigoma halafu ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hili la ligi kuu msiniulize itakuwaje ila ni lazima tutalichukua hata kama wao ndio watatangazwa mabingwa.”

SOMA NA HII  MECHI YA SIMBA NA YANGA MCHEZAJI AFARIKI UWANJANI...TUKIO HILI LINASIKITISHA SANA!