Home Uncategorized KOCHA YANGA: KAZI BADO MPAKA UBINGWA

KOCHA YANGA: KAZI BADO MPAKA UBINGWA

 


BAADA ya kufanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa matokeo ya kumaliza mzunguko wa kwanza kwa kuwa kileleni yanawapa chachu ya kuweza kuendeleza wimbi la ushindi katika mzunguko wa pili.

 

Yanga wamefanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa vinara wa ligi, wamepata pointi 43 kupitia michezo 17, wameshinda 13 na sare nne huku na hawajapoteza mchezo wowote.

 

Kaze amesema, amefurahishwa na matokeo ya ushindi dhidi ya Ihefu kwa ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wake wa kufungia mzunguko wa kwanza.


Jambo hilo amesema litawafanya wazidi kupambana ili kuwa bora kwenye mechi zao zijazo ambazo ni za mzunguko wa pili.

 

“Tunashukuru kuweza kumaliza mzunguko wa kwanza tukiwa tunaongoza msimamo wa ligi, hii ni kutokana na wachezaji kujitoa na kujitambua kuhakikisha tunapata pointi tatu katika kila mchezo ambazo zimetufikisha hapa.

 

“Ni matumaini yetu tutaanza vyema mzunguko wa pili ili tuweze kufanikiwa kufanya vizuri ili mwisho wa siku tuweze kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi,” amesema Kaze.

SOMA NA HII  LA LIGA, M-Bet, KUWAPIGA MSASA MAKOCHA