Home Azam FC ISHU YA BEKI MGHANA KUIBUKIA YANGA IPO HIVI

ISHU YA BEKI MGHANA KUIBUKIA YANGA IPO HIVI

[the_ad id="25893"]

 UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umebainisha kuwa hawajapata ofa yoyote kutoka Yanga inayomujitaji beki wao Yakub Mohamed.

Yakub raia wa Ghana amekuwa akitajwa kuingia rada za Yanga kwa ajili ya kutumika hapo msimu wa 2021/22.

Sababu kubwa za Yanga kuhitaji saini yake ni kumpata mbadala wa Lamine Moro ambaye amekuwa akisumbuana nao katika suala zima la nidhamu.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa hawajapata ofa yoyote kutoka Yanga na isitoshe mchezaji huyo ana mkataba.

“Hatujapata ofa yoyote kutoka timu yoyote kwa sasa hizo unazosikia ni tetesi, pia mchezaji bado ana mkataba na Azam FC,”.

Chanzo: Championi.

SOMA NA HII  REKODI ZA AZAM FC NDANI YA LIGI KUU BARA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here