Home Makala ISHU YA KUBEBA MATOKEO IWEKWE KANDO, WACHEZAJI CHEZENI

ISHU YA KUBEBA MATOKEO IWEKWE KANDO, WACHEZAJI CHEZENI


 KAZI kubwa kwa mashabiki Julai 3 ambapo kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga iwe ni kushangilia mwanzo mwisho bila kuleta bugudha kwa kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa.


Imekuwa kawaida kwa mashabiki wa kila timu kuvuta kamba kwao wakiamini kwamba wanakwenda kushinda licha ya kwamba hawajui maandalizi yapoje na hali za wachezaji zipo kwenye wakati upi.


Ikumbukwe kwamba mchezo huo awali ulipangwa kuchezwa Mei 8 hivyo kwa sasa maisha yangekuwa yanaendelea ila kutokana na sababu mbalimbali ngoma ikayeyuka na Julai 3 inatarajiwa kuchezwa tena.


Kwa kuwa sasa ipo wazi na kila mmoja anatambua kwamba kuna mchezo mkali unakwenda kuchezwa basi kila mmoja ajiandae kisasikolojia kuweza kupata kile ambacho anakistahili.


Kikubwa ambacho kinahitajika kwa mashabiki ambao watajitokeza Uwanja wa Mkapa kuacha kubeba matokeo uwanjani. Kubeba matokeo mfukoni kutawafanya wapate kile ambacho hawajakitarajia


Mchezo wa mpira ikumbukwe kwamba ni mchezo wa makosa wale ambao wataamini kwamba watashinda na kisha wakafungwa basi itakuwa ni maumivu kwao.


Mashabiki ambao watabeba matokeo mfukoni huwa inakuwa ngumu kwao kuamini kile ambacho watakiona baada ya dk 90 kukamilika hivyo jambo la msingi ni kujiandaa kusubiri matokeo uwanjani.


Hakuna mchezaji ambaye anapenda kuona timu yake ikifungwa hilo lipo wazi lakini unapozungumzia maisha ya soka kila kitu kinawezekana kwa namna yoyote ile.


Ile timu ambayo inaamini kwamba ni bora na ina kila kitu inaweza kufungwa tena mabao mengi na timu ambayo haipewi nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wao.


Ushindani ni mkubwa hilo lipo wazi na kila mmoja anahitaji kupata matokeo hivyo jambo la msingi ni kusubiri na kuona baada ya dk 90 nini kitatokea kwa kuwa kila timu ina nafasi ya kushinda.


Kikubwa ambacho kinahitajika ni maandalizi mazuri kwa timu kiujumla kuanzia wakati huu mpaka muda wa mechi kila kitu kiwe kwenye mpangilio mzuri na hiyo itasaidia kuleta matokeo chanya.


Wachezaji kwenye mechi za hivi karibuni tumeona kwamba wamekuwa na ubabe mwingi ndani ya uwanja hili halipo sawa na muhimu ni kujipanga kwa umakini katika kusaka matokeo.

SOMA NA HII  HII NDIO AVIC TOWN....SEHEMU WALIPOJIFICHA YANGA ...KIBONGO BONGO UNAWEZA KUDHANI NI ULAYA AISEE...


Ikumbukwe kwamba kila mchezaji ni mlinzi wa mchezaji mwingine hapo kinachotakiwa ni nidhamu pamoja kuamini kwamba wote ni ndugu na sio maadui.


Sakeni pointi tatu bila kuumizana kwani kwa sasa huu ni mzunguko wa pili na wa lala salama mchezaji akipata maumivu wakati huu itamfanya akae nje ya uwanja kwa muda mrefu.