Home Yanga SC MABOSI YANGA WAMALIZANA NA JEMBE LA KAZI KUTOKA CONGO

MABOSI YANGA WAMALIZANA NA JEMBE LA KAZI KUTOKA CONGO

 


RASMI mabosi wa Yanga wamekamilisha dili lao la kumsainisha nyota wa AS Vita, Djuma Shaban kwa kandarasi ya miaka miwili.

Hivi karibuni Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga alikwea pipa kuelekea DR Congo ambapo ilielezwa kuwa alimalizana na baadhi ya nyota ikiwa ni pamoja na Djuma.


Picha ambazo zimesambaa leo katika mitandao ya kijamii zimemuonyesha beki huyo akimwaga wino na moja akiwa na Injinia.

Kuhusu usajili wa msimu huu Injinia aliweka wazi kwamba watafanya usajili mzuri ambao utakuwa ni wa kisasa kabisa.

Taarifa zimeeleza kuwa nyota huyo atajiunga na Yanga msimu ujao wa 2021/22 atatambulishwa rasmi siku ya Wananchi.

SOMA NA HII  YANGA YAPENYA 16 BORA MBELE YA TANZANIA PRISONS