Home EURO 2020 MICAH RICHARDS AIONYA ENGLAND MBELE YA ITALY

MICAH RICHARDS AIONYA ENGLAND MBELE YA ITALY


BEKI wa zamani wa klabu ya Manchester City na timu ya Taifa ya England, Micah Richards amewataadharisha nyota wa timu ya Taifa ya England kuwa makini katika mchezo wao wa fainali dhidi ya Italy.

Richards ambaye amewahi kufanya kazi chini ya kocha wa sasa wa Italy, Roberto Mancini akiwa na klabu ya Man City, amesema anahofu sana juu ya uwezo wa kocha wake huyo wa zamani, hasa anapowaandaa wachezaji wake na michezo mikubwa.

England leo Jumapili itawavaa Italy katika mchezo wa fainali wa michuano ya Euro 2020, itakayopigwa kwenye uwanja wa Wembley nchini England.

Akizungumzia uwezo wa Mancini, Richards amesema: “Mancini ni miongoni mwa makocha wenye uwezo mkubwa sana wa kutengeneza saikolojia za wachezaji wake hasa kuelekea michezo mikubwa, hivyo nadhani England wanapaswa kuwa makini sana kwenye mchezo huo wa fainali.

“Naweza kuyasema haya kwa kuwa nimewahi kuwa chini yake, na nakumbuka vitu vingi kumhusu na mafanikio makubwa niliyopata chini yake.”


 

SOMA NA HII  URENO YATINGA 16 BORA, RONALDO NA MSHIKAJI WAKE BENZEMA WAKIWASHA