Home Yanga SC MZEE MPILI: TAWI LA IKWIRIRI LINACHEZA MPIRA WA YANGA, KIGOMA TUNAPATA MATOKEO

MZEE MPILI: TAWI LA IKWIRIRI LINACHEZA MPIRA WA YANGA, KIGOMA TUNAPATA MATOKEO


 HAJI Omar ‘Mzee Mpili’ amefunguka kuwa amezungumza na baadhi ya viongozi wa Yanga akiwemo Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msola na Injinia Hersi juu ya mwenendo wa klabu.

 

Mzee Mpili ambaye ni mwanachama wa Klabu ya Yanga kwa siku za hivi karibuni alijivunia umaarufu mkubwa baada ya kumalizika kwa mchezo wa Simba dhidi ya Yanga uliopigwa Julai 3, mwaka huu.

 

Umaarufu huo ulikuja ambapo kabla ya mchezo huo alitamba kuifunga Simba na hatimae jambo hilo likatimia baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

 

Aliyazungumza hayo kwenye kipindi maalum ambacho kilifanyika jana kwenye Ofisi za Global Publishers kupitia kipindi maalum kilichoruka kupitia Global TV na +255 Global Radio.

 

“Nimeanzisha mradi wa kuuza t-shirt kwa ajili ya kuchangia tawi langu la Ikwiriri, nikaamua kutoa t shirt hizi katika kuhakikisha kazi inamalizika kigoma.


“Tawi la Ikwiriri ndio linacheza mpira kutokana na namna ambavyo mimi nimeleta morali kwenye klabu, mshikamano nimeleta na kigoma tunapata matokeo ndani ya uwanja.

 

“Nakaa upande wa wachezaji katika kuchezesha na ninapata nafasi ya kuzungumza na wachezaji kutokana na kutambulika kwani kila mtu ananijua ndani ya Yanga pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

 

“Niliwaambia wachezaji watulie na kupata nafasi ya kucheza, Simba wanatumia ndani na nje ya uwanja, nasema mpira ni dakika 90 za ndani ya Uwanja ila sisemi natumia njia gani katika kucheza mpira.

 

“Simba walikuwa wanakaa vizuri kwa mshikamano niliwahi kuwaambia Yanga kuwa hawashirikiani na endapo watashirikiana kwa pamoja basi timu itafanya vizuri, mara kila mtu analeta wachezaji wake hii inaleta shida,” .

Julai 25, Yanga inatarajia kucheza na Simba, Uwanja wa Lake Tanganyika kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni fainali.

SOMA NA HII  YANGA YATAMBA KUFIKIA REKODI YA SIMBA KAGAME