Home Simba SC NYOTA WANNE WA SIMBA KUIKOSA COASTAL UNION LEO KWA MKAPA

NYOTA WANNE WA SIMBA KUIKOSA COASTAL UNION LEO KWA MKAPA

 


IKIWA leo kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kinatarajiwa kucheza mbele ya Coastal Union nyota wake wanne wataukosa mchezo wa leo kutokana na sababu mbalimbali.

Nyota hao ni pamoja na kiungo Bernard Morrison ambaye huyu kwa mujibu wa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ana matatizo ya kifamilia hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi.

Morrison alikuwepo kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Yanga na aliyeyusha dk zote 90 wakati akishuhudia mabosi wao wa zamani wakiwatungua bao 1-0 pia kwenye mchezo dhidi ya KMC aliyeyusha dk 5 wakati aliposshuhudia timu yake ikishinda mabao 2-0.

Pia Ibrahim Ajibu kiungo huyu hayupo kambini kwa kile ilichoelezwa kwamba ana malaria.

Nyota mwingine ni Jonas Mkude huyu ni ishu ya nidhamu ambayo imemuweka nje ya kikosi hicho na nyota wa nne ni kiungo Perfect Chikwende ambaye yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa.

Pia kwenye kikosi cha leo huenda Gomes akafanya mabadiliko kwa kuanzisha wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi ili kuweza kuonyesha uwezo wao na miongoni mwa nyota ambao wanatarajiwa kuanza ni pamoja na Miraj Athuma, Said Ndemla ambao wamekuwa hawapati nafasi kikosi cha kwanza.

SOMA NA HII  KUHUSU KUWAACHA MZAMIRU NA ONYANGO....SIMBA WAIBUKA NA HILI TENA....AHMED ALLY AGUSIA YA MO DEWJI...