Home Yanga SC RASMI : ALICHOKISEMA MAKAMBO KUHUSU DILI LAKE LA KURUDI YANGA

RASMI : ALICHOKISEMA MAKAMBO KUHUSU DILI LAKE LA KURUDI YANGA

 


STRAIKA kipenzi wa mashabiki wa Yanga, Heritier Makambo ametamka kauli ambayo mashabiki wa klabu hiyo walikuwa wanaisubiri kwa hamu.

Makambo ambaye ni raia wa DR Congo aliyemwagana na AC Horoya ya Guinea, ameliambia gazeti la Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka nje kidogo ya Jiji la Kinshasa kwamba: “Nakuja Yanga.” Mwanaspoti linajua kwamba kila kitu baina ya Yanga na mchezaji huyo kipo kwenye hatua za mwisho na baadhi ya vigogo wamepania kumshusha Dar kwa kishindo ingawa kuna baadhi wanaihofia Azam huenda ikatia mkono.

Mchezaji huyo amekiri kwamba kuna mazungumzo mazuri baina yake na Yanga na kama yakikamilika muda wowote atakuja kuishia pale alipoishia maana Jangwani ni nyumbani kwake.

Kabla ya kutimka Yanga akiuzwa Horoya, Makambo alikuwa staa mkubwa akifunga mabao 17 katika ligi ambapo licha ya Yanga kukosa ubingwa wala kombe lolote, lakini aliibuka kuwa mfungaji bora wa kikosi hicho cha kocha wa wakati huo, Mwinyi Zahera Mkongomani mwenzake.

Makambo aliuzwa Horoya kwa Euro 70,000 akiwa ameitumikia Yanga mwaka mmoja pekee katika miaka miwili aliyosaini ambapo hata hivyo akiwa nchini Guinea alishindwa kutamba katika miaka yake miwili ya kwanza kabla ya wiki hii kuvunja mkataba na mabingwa hao wa nchini humo na wakaachana kiroho safi akasepa zake DR Congo.

“Siwezi kukataa kurejea Yanga, hiyo ni klabu ambayo ilinitambulisha karibu sehemu kubwa, nawakumbuka sana watu wa Yanga, ni kweli nipo katika mazungumzo na viongozi,” alisema Makambo ambaye alitamba na staili yake ya kushangilia ya kuwajaza akipiga viganja vyake viwili huku mikono akivinyoosha kila alipofunga bao.

SOMA NA HII  HATIMA YA DJUMA NA YANGA HADHARANI, ISHU IKO HIVI