Home Habari za michezo MSAUZI KUPEWA U-CEO SIMBA….KAJULA AANZA KUAGA WACHEZAJI….ISHU NZIMA IKO HIVI…

MSAUZI KUPEWA U-CEO SIMBA….KAJULA AANZA KUAGA WACHEZAJI….ISHU NZIMA IKO HIVI…

Habari za Simba SC

UONGOZI wa Simba wapo kwenye mchakato wa kutafuta Mtendaji Mkuu kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya kuja kuchukuwa nafasi ya Iman Kajula ambaye amekubalia kuachia ngazi.

Hatua hiyo ni baada ya hivi karibuni kufanyika kikao kizito kutathimini mikakati na mwenendo mbaya wa timu hiyo kwa sasa.

Maamuzi yamefanyika tayari Mtendaji Mkuu Kajula amekubali kuachia nafasi yake na klabu inatarajia kumleta CEO mpya kutoka Afrika Kusini.

Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo ameeleza kuwa Kajula alienda juzi mazoezi ya timu hiyo kabla kwenda Zanzibar kwa ajili ya kuangana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi.

“Ni kweli kule kutembelea timu lengo ni kuwaaga wachezaji na benchi la ufundi kwa sababu tayari amekubali kuachia ngazi nafasi yake, huku mchakato ukiendelea wa kuleta mtu kutoka Afrika Kusini,” amesema chanzo hicho.

Amesema wameanza na mtendaji mkuu na pia maboresho yanatarajiwa kufanywa ndani ya uongozi huo na kuhakikisha klabu hiyo inarejesha heshima yake katika soka la ndani.

Kajula ambaye alipewa majukumu hayo kwa miezi sita baada ya Barbara Gonzalez kuachia ngazi kwa ajili ya kutafuta changamoto zingine nje ya Simba

SOMA NA HII  MBRAZILI AENDELEA KUIPASUA KICHWA SIMBA....UBUTU WA BOCCO,PHIRI NA BALEKE WAMTIA WAZIMU...