Home Yanga SC SAIDO AWAGAWANYA MABOSI YANGA, WENGINE WATAKA ASEPE MAZIMA

SAIDO AWAGAWANYA MABOSI YANGA, WENGINE WATAKA ASEPE MAZIMA


 VIONGOZI wa Yanga wamejikuta wakiwa katika njia panda mara baada ya kupatwa na kigugumizi cha kuachana au kubaki kwa mshambuliaji wao, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’.


Ntibazonkiza alijiunga na 
Yanga katika usajili wa dirisha dogo uliofanyika Januari 2021 ambapo mpaka sasa ameitumikia klabu hiyo kwa nusu msimu.

 

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, viongozi hao mpaka sasa wameshindwa kutoa maamuzi juu ya mchezaji huyo asalie au aachwe ambapo wanaotoka aondoke wametaja sababu ni wingi wa idadi ya wachezaji wa kimataifa ambao unahitaji kuwasajili lakini pia ishu ya majeraha ya mara kwa mara.

 

“Uongozi wa Yanga unashindwa kuamua hatima ya Saido kuwa asalie au aondolewe, kama ambavyo unamuona kuwa mchezaji huyo chini ya kocha Nasreddine Nabi ameshindwa kabisa kutamba katika kikosi cha kwanza huku mara nyingi akiwa katika wachezaji wa akiba.


“Lakini pia ishu ya majeraha ya mara kwa mara ambayo amekuwa akikumbana nayo Saido na kumfanya acheze michezo michache pia imekuwa ni sababu kubwa inayomfanya mchezaji huyo kuufanya uongozi wa kufikiria uwezekano wa kuvunja mkataba wake huku viongozi wengine wakitaka mchezaji huyo asalie,” kilisema chanzo hiko.

 

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Dominick Albinus kuhusu hatma ya mchezaji huyo, alisema kuwa wachezaji wote wa Yanga ambao watasalia ndani ya Yanga na ambao wataondoka basi taarifa itatolewa na uongozi wa timu kama ambavyo taarifa nyingine zilitolewa.

 

“Siwezi kusema lolote kuhusu hilo kwani taarifa zote za wachezaji ambao wanasajiliwa na wale watakaoachwa zitatolewa na utaratibu maalumu wa timu kama ambavyo imetokea katika utolewaji wa taarifa zilizopita,” alisema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  MUKOKO..NTIBAZONKIZA KIKAANGONI YANGA...NABI AKABIDHIWA RUNGU LA MAAMUZI..INJINIA HERSI AWAKATA KIAINA...