Home Simba SC SIMBA vs YANGA| HIZI HAPA REKODI ZITAKAZOMBEBA GOMES NA SIMBA YAKE LEO

SIMBA vs YANGA| HIZI HAPA REKODI ZITAKAZOMBEBA GOMES NA SIMBA YAKE LEO


Simba na Yanga zitavaana leo, huku timu zote zikijifua vilivyo na mazoezi ya juzi jioni ya Simba, yaliyofanyika Mo Simba Arena, vigogo kuanzia Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalen, Mohammed Nassor ‘Mkigoma’ na Crescentius Magori walitinga kuwapa mzuka zaidi nyota wao chini ya Gomes.

Uwepo wa vigogo hao walifanya tizi la Simba kuwa la kibabe, lakini rekodi zikionyesha Gomes hajapoteza mechi yoyote ya Ligi Kuu tangu alipojiunga na timu hiyo, huku ubabe wake kuna wanaume nane waliomlainisha kazi yake.

Gomes ameiongoza Simba katika michezo 14 ya Ligi kati ya hiyo ameshinda 12 na kutoka sare mbili, huku vijana wake wakifunga mabao 32 na kuruhusu sita tu.

Jambo ambalo pengine hulifahamu, katika idadi hiyo ya mabao 32 ambayo Simba imeyafunga kwenye Ligi Kuu ikiwa chini ya Gomes, yamefungwa na wachezaji nane tu tofauti na ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Sven Vandenbroeck ambaye chini yake licha ya Simba kupachika jumla ya mabao 37 katika Ligi Kuu msimu huu, idadi ya wachezaji 13 walishiriki kupachika mabao hayo.

Wachezaji hao ni John Bocco, Luis Miquissone, Clatous Chama, Medie Kagere, Chris Mugalu, Bernard Morrison, Rally Bwalya na Mohamed Hussein

Mtu anayeonekana kunufaika zaidi na mbinu za Gomes ni mshambuliaji Luis Miquissone ambaye ndiye anaongoza kwa kufunga idadi kubwa ya mabao katika Ligi Kuu chini ya Gomez akiwa amefunga jumla ya mabao nane.

Miquissone anafuatiwa na nahodha John Bocco na Chris Mugalu ambao kila mmoja amepachika mabao sita kwenye Ligi Kuu huku Medie Kagere akiwa amefunga jumla ya mabao manne wakati Bernard Morrison amefunga mabao matatu chini ya Mfaransa huyo.

Wachezaji wengine watatu waliofunga mabao kwenye Ligi Kuu tangu Simba ilipoanza kunolewa na Gomes ni Rally Bwalya na Clatous Chama ambao kila mmoja amefunga mabao wawili wakati huohuo Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akiwa amepachika bao moja.

Hiyo ni tofauti na ilivyokuwa katika mechi 15 za mwanzo za Ligi Kuu msimu huu ambazo Simba iliongozwa na Vandenbroeck kwani jumla ya wachezaji 13 walishiriki katika kupachika jumla ya mabao 37 ambayo timu hiyo ilifunga ikiwa na kocha huyo ambaye kwa sasa anainoa FAR Rabat ya Morocco.

SOMA NA HII  MHHHH....KWA HILI LA MANULA HAPANA AISEEE....KUNA JAMBO HALIKO SAWA TOKA 5G YA YANGA...

Luis akitamba chini ya Gomes, enzi ya Vandenbroeck mchezaji aliyeng’ara zaidi ni nahodha John Bocco ambaye alipachika jumla ya mabao nane akifuatiwa na Kagere aliyefunga mabao saba na nyuma yao alikuwa ni Clatous Chama aliyefumania nyavu mara sita.

Chini ya Sven, Mzamiru Yassin, Said Ndemla na Hassan Dilunga kila mmoja alipachika mabao mawili na Miquissone, Morrison, Mohamed Hussein, Joash Onyango, Pascal Wawa na Ibrahim Ajibu kila mmoja akifunga bao moja.

Miongoni mwa vitu ambavyo Gomes ameviendeleza kutoka kwa Sven ni kumtumia John Bocco kama silaha yake kuu kwa mechi za ugenini kwani mshambuliaji huyo ndiye mchezaji aliyefunga idadi kubwa ya mabao katika viwanja vya ugenini akifanya hivyo mara nne akifuatiwa na Bernard Morrison na Mugalu ambao kila mmoja amefunga mabao matatu.

Katika mechi za nyumbani, Gomez amekuwa akimtegemea zaidi Miquissone ambaye amefunga mabao matano akifuatiwa na Kagere matatu.

Simba chini ya Gomes imekuwa tishio katika kufumania nyavu katika vipindi vyote vya mchezo na kuthibitisha hilo, imefunga idadi sawa ya mabao katika kila kipindi, mabao 16 kipindi cha kwanza na mengine 16 kipindi cha pili.

Hiyo ni tofauti na nyakati za Sven ambapo Simba ilikuwa tishio zaidi katika kipindi cha kwanza ilifunga 21, kipindi cha pili mabao 16.

Mchambuzi wa soka, George Ambangile alisema Gomes ameifanya Simba icheze kwa majukumu zaidi jambo ambalo linawafanya idadi ndogo ya wachezaji ifunge tofauti na ilivyokuwa wakati wa Sven

“Chini ya Sven, Simba walikuwa wanacheza kwa kushiriki timu nzima (total football) tofauti na sasa wakati wa Gomes.

wanacheza soka la kimajukumu, kuna watu wapo kwa ajili ya kushambulia ambao ni washambuliaji na viungo washambuliaji na ndio maana unaona ndio wanaofunga mabao mara kwa mara,” alisema Ambangile.