Home Habari za michezo KUMBE HIKI NDIO CHANZO CHA SIMBA KUFUNGWA NA YANGA…ISHU NZIMA A-Z HII...

KUMBE HIKI NDIO CHANZO CHA SIMBA KUFUNGWA NA YANGA…ISHU NZIMA A-Z HII HAPA

Habari za Yanga leo

Mchambuzi wa masuala ya soka kutoka EFM Radio, George Ambangile amesema kuwa mchezaji aliyevuruga mfumo wa Simba SC kwenye dabi ya Kariakoo ni mshambuliaji wa Yanga, Joseph Guede.

George amesema hayo baada ya Simba kupokea kichapo cha bao 2- 1 kutoka kwa watani zao Yanga SC, Aprili 20, 2024 huku Guede akifunga bao la 2 katika mchezo huo mkubwa barani Afrika.

“Joseph Guede ndo alietengeneza matatizo yote kwa Simba SC maana kwa hali ya kawaida unajua Guede sio mnyumbulifu kama Mzize na Musonda, kwa hio mimi kama center back najua kabisa Guede atakaa kati kati yetu.

“Lakini hapana alikua anakaa kati kati ya center back na full back, kwa hio alikua anaivuruga sana backline ya Simba hawajui Zimbwe Jr amsongelee Guede kwa maana akifanya hivyo anafinya uwanja then kuna space inafunguka kwa full back wa Yanga.

“Center back mmoja akimsongelea kuna space pia inafunguka kwa kina Max kutumia ilikua trick sana hata goli alilofunga alikua kati kati ya Tshabalala na Che Malone na wote walikua hawajui nini wafanye mpaka kwa lugha ya picha che Malone alionekana akisema kwa nini hatuongei, Guede alikua bora sana,” amesema Ambangile.

SOMA NA HII  MGUNDA ATUNISHA KIFUA SIMBA..."MECHI NA AZAM NI FAINALI...AFUNGUKA HAYA