Home Habari za michezo MGUNDA ATUNISHA KIFUA SIMBA…”MECHI NA AZAM NI FAINALI…AFUNGUKA HAYA

MGUNDA ATUNISHA KIFUA SIMBA…”MECHI NA AZAM NI FAINALI…AFUNGUKA HAYA

Habari za Simba SC

kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda amesema kuwa anaamini ataisaidia timu hiyo kurejea katika makali yake ambayo imeyapoteza kwa siku za hivi karibuni baada ya kutetereka na kutopata matokeo chanya.

Mgunda ambaye amechukua mikoba ya Benchikha amesema hayo leo wakati akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam Fc.

“Tunakutana na Azam FC, mchezo utakuwa mgumu sana na tunaweza kusema ni fainali kwa sababu ndio unaotoa taswira ya kushika nafasi ya pili kwa sababu tunahitaji kumaliza kwenye nafasi hiyo.

“Si rahisi, lakini naamini nitaisaidia Simba SC irudi kwenye ushindani, nina imani wachezaji watairudisha timu sehemu nzuri. Vijana waliopo wote wamepevuka na wanaelewa namna ya kufanya ili kuiweka timu katika ushindani, hivyo cha muhimu ni kuwajenga kisaikolojia na kuwarudisha kwenye morali na kila kitu kitakuwa sawa,” amesema Mgunda.

SOMA NA HII  MMH YANGA YAIBUKA NA MIKAKATI HII HATARI...RAIS AMEFUNGUKA HAYA