Home Habari za michezo MATOLA :- TUNAENDA KUTIBUA REKODI IVORY COAST….MECHI NI NGUMU MNOOO…

MATOLA :- TUNAENDA KUTIBUA REKODI IVORY COAST….MECHI NI NGUMU MNOOO…

Habari za Simba Leo

KOCHA Msaidizi wa Simba, Selemani Matola ametamba kuwa wamekwenda nchini Ivory Coast kwa kazi mbili, kushinda mechi ya kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini pia kutibua rekodi ya wapinzani wao ambao hawajapoteza mechi yoyote kwenye Kundi B.

Simba iliondoka usiku wa kumkia jana kuelekea nchini humo ikiwa na lengo la kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo, na moja kati ya walichokiangalia ni kutoruhusu bao katika mchezo huo utakaochezwa uwanja wa uwanja wa Felix, Houphouel- Boign, Ijumaa ya Februari 23, mwaka huu.

Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema benchi la ufundi na wachezaji wanatambua ugumu wa mechi hiyo na wamejiandaa vizuri kwa ajili ya kupambania timu kupata matokeo chanya.

Amesema ugumu wa Asec Mimosas ni kupata rekodi nzuri katika michuano hiyo kwa kuongoza kundi hilo lakini wamejiandaa kutibua rekodi hiyo kwa kutoruhusu kufungwa katika mchezo huo na kutumia nafasi zinazopatikana.

“Tumewaangalia Asec Mimosas hivi karibuni tunaenda kucheza na timu ngumu , kuendeleza rekodi yake lakini kwa upande wetu tumejipanga vizuri safu ya ulinzi kuwa makini na washambulia wa wapinzani na washambuliaji wetu kupewa amjukumu ya kuhakikisha tunavuna alama muhimu katika mchezo wetu.

Kurejea kwa beki wetu, Henock Inonga ni jambo zuri kwa sababu anazidi kuimarisha safu ya ulinzi kwa kutibua mipango yao na kupambana kutafuta pointi ugenini na kuja kushinda katika mechi yetu ya nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy ,” amesema Matola.

Ameongeza kuwa wakifanikiwa kupata alama Asec Mimosas na kushinda mechi yao ya nyumabini , watafikia malengo yao ya kufuzu na kwenda kucheza robo fainali ya michuano hiyo.

Kuhusu kukosekana kwa kipa wao Ayoub Lakred kutokana na kutumia adhabu ya kadi, Matola alisema hawana presha sana juu ya kumkosa nyanda huyo kwa sababu katika nafasi hiyo ina watu na kuweza kufanya vizuri.

“Tunamkosa Ayoub lakini kulingana na ubora wa makipa wetu hatuna presha kwa sababu tuna Manula (Aishi), Ally (Salim) ambao wako vizuri na kusaidia timu kufikia malengo yetu ya kupambania timu kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Matola.

Ameeleza kuwa wataendelea kuzungumza na wachezaji wangu kuhusu nidhamu uwanjani ikiwemo kuwa makini kutopata kadi za kuzembe licha ya hakuna mchezaji anayependa kuona anapata adhabu ya kadi.

Naye beki wa Simba, David Kameta (Duchu) amesema wako tayari kwa mchezo dhidi ya Asec Mimosas, hautakuwa mchezo rahisi wanaenda kupambana na kufuata maelekezo ya benchi la ufundi kuvuna pointi muhimu katika mchezo huo.

“Benchi la ufundi tayari wamekamilisha kazi jukumu kubwa limebaki kwetu kutafuta matokeo chanya ukizingatia kila mmoja ndani ya kundi letu tuna nafasi ya kwenda kucheza robo kwa sababu tunataka alama muhimu hapa na kwenda kushinda nyumbani,” amesema Duchu.

Amesema wanapambana kutafuta pointi tatu au moja ugenini dhidi ya Asec Mimosas na baadae wanarejea nyumbani kutafuta alama tatu muhimu watakaocheza uwanja wa nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy .

Katika kundi B, Asec Mimosas anaongoza akuwa na pointi 10, Simba ikishika nafasi ya pili kwa alama 5, Jwaneng Galaxy wana alama 4 na Wydad Casablanca wakishika mkia katika kundi hilo wakikusanya pointi tatu .

SOMA NA HII  KAMA KAWA..NABI KABAMBWA CHAMAZI AKIIPIGA CHABO SIMBA AISEE...ALIJIPIGA NGUO NYEUSI ASITAMBULIKE...