Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA JWANENG …AHMED ALLY AWAPA YANGA JINA JIPYA ….

KUELEKEA MECHI NA JWANENG …AHMED ALLY AWAPA YANGA JINA JIPYA ….

Habari za Simba leo

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema klabu yao kuingia hatua ya Robo Fainali Klabu Bingwa wameshazoea tofauti na watani wao YangaSC.

Amesema kwao ni vitu vya kawaida tofauti na watani zao ambao wameshangilia sana baada ya juzi kufuzu kwa kuwafunga CR Belouzdad.

“Yanga wanashangilia sana kuingia Robo fainali lakini sisi ni maisha yetu haya na tumeshazoea, tunawakaribisha kwenye huu ulimwengu wetu,” alisema Ahmed.

Wakati Simba wakifanya kila jitihada kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa mwisho wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Imeonekana kuwa kuna watu wanaoiombea vibaya timu ya Simba isipenye hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Meneja wa Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally anasema

“Wazandiki wanatuombea tusiende robo fainali ya mashindano ya Ligi ya mabingwa wanataka kwenda pekee yako hii ni roho mbaya tunawaambia hawana namna yoyote yakumzuia Simba SC Isiende robo fainali hii vita ni kubwa tunacheza na Waydad na Jwang Galaxy , wenye roho mbaya”

SOMA NA HII  SIMBA YAHAMA KAMBI YA 1-0...WAWEKA ULINZI MKALI...YANGA WACHEEKAA...MWANASPOTI LEO...