Home Habari za michezo NZEGELI ATOA KAULI TATA, WAPINZANI TUMBO JOTO

NZEGELI ATOA KAULI TATA, WAPINZANI TUMBO JOTO

Habari za Yanga

Nyota wa Yanga, Maxi Nzengeli ametaja nguzo tano zinazowapa wachezaji nguvu ya kupata matokeo kwenye mechi za kitaifa na kimataifa wawapo uwanjani.

Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, Yanga imetinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwenye mechi nne ambazo ni dakika 360 Yanga ilishinda mechi zote nje ndani dhidi ya ASAS FC kwa jumla ya mabao 7-1 dhidi ya AL Merrikh kwa jumla ya mabao 3-0.

Nguzo hizo ni Mungu, mashabiki, mazoezi, benchi la ufundi pamoja na uongozi wa timu hiyo kuwa nao bega kwa bega kwenye kila hatua.

Maxi Nzengeli kiungo wa Yanga mwenye mabao matatu kwenye ligi na ametupia mabao mawili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya ASAS FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Nyota huyo amesema watazidi kupambana kwenye mechi za ligi pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika kupata matokeo chanya na kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo.

β€œKikubwa ni Mungu ambaye anatupa nguvu ya kufanya kazi kwenye mechi zetu ambazo tunacheza pia mazoezi kwa ajili ya kila mechi ni muhimu hivyo baada ya mchezo tunarejea kwenye uwanja wa mazoezi kuanza maandalizi mengine.

β€œBenchi la ufundi ambalo tupo nalo wao wanatupa mbinu ambazo zinatupa matokeo. Bila kusahau uongozi ikiwa ni Rais Injinia Hers Said na mashabiki hawa ni muhimu tunapenda kuona wanajitokeza kwenye kila mechi,”.

Kwenye ligi Yanga ina pointi 12 baada ya kucheza mechi 5. Katika Ligi ya Mabingwa Afrika ipo kundi D ikiwa na Al Ahly, Madeama na CR Belouizdad

SOMA NA HII  EYMAEL: KUIFUNGA SIMBA MBELE YA JPM NI KUMBUKUMBU KWANGU NA WACHEZAJI