Home Habari za michezo JEMEDARI:- CHAMA AKIZIDIWA UWEZO UWANJANI ANAFANYAGA MAMBO YA KISHAMBA SANA…

JEMEDARI:- CHAMA AKIZIDIWA UWEZO UWANJANI ANAFANYAGA MAMBO YA KISHAMBA SANA…

Habari za Michezo leo

Ameandika mchambuzi Jemedari Said; Chama katika Ubora wa USHAMBA wake hanaga huruma na wachezaji wenzie anapozidiwa kiwanjani”

Tarehe 13 Mei 2023 nilimuambia Clatous Chota Chama kwamba jambo alilolifanya kwa mchezaji wa RUVU Shooting pale Chamazi Complex siku ya nyuma yake yani tarehe 12 Mei 2023, ilikuwa ni tukio la KISHAMBA na alikustahiki kufanywa na mchezaji kama yeye ambaye amejijengea sifa kubwa na mapenzi kwa mashabiki wa soka nchini.

Lakini alijibu kwa nyodo na jeuri na kusema lilikuwa jambo dogo sana na kama nia yake ilikuwa kumuumiza mbona aliendelea kucheza mpaka mwisho. Majibu ya kitoto kabisa, ajabu alipata uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki ambao binafsi nawaona kama mazezeta hivi.”

Lakini nikamuonyesha tukio jingine ambalo alilifanya msimu wa nyuma yake pale alipomkanyaga Feisal Salum akiwa Yanga SC bila mpira kwa makusudi rafu ambayo inaweza kumaliza muda wa kucheza wa mchezaji mwenzio.”

Jana tarehe 20 April 2024, Mwamba wa Lusaka amerudia USHAMBA uleule kwa Nickson Kibabage kwa kukanyaga bila mpira kwa rafu ambayo ingeweza kumaliza maisha ya kucheza mpira ya kijana huyu.”

Narudia tena kusema kwamba Watanzania mashabiki wa mpira wanampenda mno Chama, mimi pia nafurahia mambo ya kiufundi anayofanya kiwanjani, lakini anapofanya huu USHAMBA ni lazima kumuambia na tunapomuambia haina maana kwamba tunamchukia yeye au klabu yake, tunazichukia hızı tabia za kishamba ambazo sio za kiuanamichezo. Wachezaji wanapaswa kulindana kiwanjani sio kufanyiana faulo za kishamba kama hizi.

Siku mechi ikikataa kama ilivyokuwa jana Mzee wangu Tripple C sio vibaya ukaomba kupumzika kujiepusha na vitu vya hovyo kama hivi. Manake hapa unajiwekea alama kwamba jana hiki ndicho kitu pekee umefanya wakati mnaburuzwa na Gongowazi ambayo ni aibu.

Pia nilipokuambia msimu uliopita sikukuonea wala kukuchukia ila niliona tabia mbaya ambayo haijifichi, kama unafurahi tukikusifia kwa mazuri, vumilia tukikukosoa kwa vitu vya hovyo na huwa hatutafuti followers ila tunakurekebisha, HUU NI USHAMBA ACHANA NAO BRO.

Kamati ya uendeshaji wa ligi itaruka na wewe kama watajielekeza vyema inabidi wasome kanuni vyema kwa matukio ya kijirudia rudia wakupe MAXIMUM PUNISHMENT.

SOMA NA HII  KUELEKEA 'GAME' NA AL AHLY...SIMBA WAIBUKA NA KAULI MPYA YA MECHI HIYO....WAARABU WAPAGAWA..