Home Simba SC UTATU WA SIMBA WATUPIA MABAO 37

UTATU WA SIMBA WATUPIA MABAO 37


 UTATU wa nyota watatu wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes umetupia jumla ya mabao 37 ndani ya ligi kuu kwa msimu wa 2020/21.


Ni Bocco yeye ni namba moja kwa utupiaji katika kikosi hicho akiwa ni mzawa pekee mwenye mabao mengi ambao ni 14.

Chris Mugalu raia wa Congo yeye ametupia jumla ya mabao 12 akiwa ni namba mbili kwa kucheka na nyavu katika kikosi hicho kinachoongoza ligi na pointi zake 76.

Kwa upande wa Mnyarwanda Meddie Kagere yeye ametupia jumla ya mabao 11 akiwa nafasi ya tatu kwa watupiaji ndani ya kikosi hicho.

Ikumbukwe kwamba Kagere ana kibarua cha kutetea tuzo ya ufungaji bora ambayo alisepa nayo msimu wa 2019/20 baada ya kutupia jumla ya mabao 22.

Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 31 imetupia mabao 71 ambayo ni mengi ndani ya ligi kwa msimu huu na inafuatiwa na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 70 ikiwa imefunga jumla ya mabao 50.

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa anafurahi kuona wachezaji wake wakifunga ndani ya uwanja kwa kuwa wanatimiza majukuu yao.

SOMA NA HII  SAKHO NAYE ANYOOSHA MIKONO SIMBA...WAKALA WAKE AGUNGUKA A-Z...AZAM FC WAHUSISHWA..