Home Simba SC WAWILI WA SIMBA KUIKOSA YANGA KESHO KWA MKAPA

WAWILI WA SIMBA KUIKOSA YANGA KESHO KWA MKAPA

 NYOTA wawili wa Simba kesho wanatarajia kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. 

Kwa mujibu wa kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa kiujumla maandalizi yapo tayari kwa ajili ya mchezo huo licha ya kuwakosa wachezaji wawili.

“Ni Jonas Mkude ambaye matatizo yake yanajulikana pamoja na Ibrahim Ajibu ambaye anasumbuliwa na Malaria.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwa kuwa kila kitu kipo sawa na wachezaji wanahitaji ushindi, ” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 73 na Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 67.

Mkude alisimamishwa na Simba kutokana na tatizo la kinidhamu ambapo anatakiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya akili.


SOMA NA HII  KISA SIMBA KUCHEZA DUBAI...KAMA KAWAIDA JEMEDARI SAID 'KALIPUKA' NA 'NONDO HIZI'...