Home Simba SC KUELEKEA DERBY KESHO: GOMES HAJUI AMUANZISHE NANI KWENYE USHAMBUALIJI

KUELEKEA DERBY KESHO: GOMES HAJUI AMUANZISHE NANI KWENYE USHAMBUALIJI


KOCHA Mkuu wa Simba Didier Gomes atakuwa na kibarua kizito cha kuamua ampange nani eneo la ushambuliaji kwenye mechi dhidi ya Yanga kutokana na uwezo walioonesha wachezaji wa eneo hilo mazoezini leo.

Chris Mugalu, John Bocco na Meddie Kagere ndio washambuliaji wa kati wa Simba ambao kwenye mazoezi yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Mo Simba Arena, walikuwa wakiwasha moto kila wakati.

Gomes aligawa wachezaji katika makundi mawili ambapo wale wanaocheza eneo la beki na kiungo mkabaji walikaa sehemu yao wakicheza mpira kwa aina tofauti chini ya kocha msaidizi Seleman Matola huku Gomes akikomaa na washambuliaji na viungo wa juu.

Katika eneo la washambuliaji na viungo wa juu, Gomes alikuwa na Bocco, Mugalu, Kagere, Benard Morrison, Clatous Chama, Luis Miquissone, Rally Bwalya, Miraji Athuman, Said Ndemla, Mzamiru Yassin na Hassan Dilunga.

Kundi hilo la wachezaji lilikuwa likicheza mbele ya goli moja la uwanja huo mahali ambapo kocha Gomes alikuwa amepanga koni vifaa maalumu virefu vya kutenganisha nafasi na kuwataka wachezaji hao kutengeneza nafasi na kufunga.

Bocco, Mugalu na Kagere walisimama kama washambuliaji watatu wa juu ambapo walikuwa wakitengenezewa nafasi za kufunga na viungo wengine huku wao wakifanya kazi ya kupiga mashuti na kumfunga Manula kwa aina mbali mbali za ufungaji.

Katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 20, washambuliaji watatu hao kila mmoja alifunga zaidi ya bao 7 huku viungo wengine wakiongozwa na Chama aliyefunga mara nne.

Simba inajiandaa kwa ajili ya mechi ya kiporo ya Ligi Kuu dhidi ya watani zao Yanga iliyopangwa kuchezwa Jumamosi kwenye dimba la Benjamin Mkapa kuanzia saa 11:00 jioni.

SOMA NA HII  IMEVUJA RASMI...BALEKE ANA MKATABA HALALI NA TP MAZEMBE...SIKU ZAKE ZINAHESABIKA SIMBA