Home kimataifa CR 7 ASEPA NA TUZO ITALIA, AFICHUA KINACHOMBEBA

CR 7 ASEPA NA TUZO ITALIA, AFICHUA KINACHOMBEBA


 NYOTA wa kikosi cha timu ya Juventus inayoshiriki Ligi Kuu ya Serie A, Cristiano Ronaldo amepewa tuzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2020 kwa wachezaji wanaocheza Italia.

Ronaldo ametwaa tuzo hiyo hivi karibuni baada ya kufanya vizuri kwa mwaka 2020 ambapo alifunga mabao 31 kwenye mechi 33 za ligi.

Pia msimu uliopita timu yake ya Juventus ilitwaa taji la Serie A na aliibuka kuwa mchezaji bora.

Baada ya kutwaa tuzo hiyo Ronaldo amesema kuwa anapenda kuwashukuru wote ambao wamehusika katika mafanikio yake kwa kuweza kupata tuzo hiyo.

“Nataka kuwashukuru wachezaji wenzangu kwani wao wamefanikisha mimi kupata tuzo hii kwa kunipigia kura.

“Bidii nguvu na kujiamini ndiyo imekuwa siri kubwa ya mafanikio yangu pamoja na nidhamu ndiyo maana nimeweza kuwa hapa nikiwa na umri wa miaka 36 naweza kufika hata 40,” . 

SOMA NA HII  HARRY KANE ANATAKA KUONDOKA SPURS