Home Yanga SC YANGA YAFUNGUKIA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO, KIGOMA

YANGA YAFUNGUKIA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO, KIGOMA


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi matarajio yao ya ushindi katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Simba, unaotarajiwa kuchezwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

 

Yanga wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya Simba katika mchezo uliokuwa wa nusu fainali ya michuano hiyo, msimu uliopita.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Hersi alisema kuwa kuelekea katika mchezo huo, watahakikisha wanashinda.“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya kuhakikisha tunaibuka na ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wetu wa fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, muhimu katika mchezo huu ambao ni wa fainali ni kubeba taji hilo.

 

“Siku zote tunasema kuwa fainali haichezwi bali fainali hushindwa, hivyo kuelekea katika mchezo huo, tunaenda kwa ajili ya kushinda fainali hiyo,” alisema kiongozi huyo.


Yanga watacheza fainali hiyo wakiwa wametoka kuichapa Simba bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu, wiki mbili zilizopita.

SOMA NA HII  PHIRI AFUNGUKA HAYA KUHUSU PENALTI ALIYOKOSA KWENYE NGAO YA JAMII