Home Yanga SC YANGA:HATUNA CHA KUFANYA

YANGA:HATUNA CHA KUFANYA

 BAADA ya kupoteza katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho, uongozi wa Yanga umebainisha kuwa kwa sasa hauna la kufanya.

Ilikuwa jana Julai 25, mwisho wa reli Kigoma ambapo ilichezwa fainali iliyoshuhudia miamba miwili ikimenyana, Simba na Yanga ambao ni watani wa jadi.

Dakika 90 zilikamilika na ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ukisoma Simba 1-0 Yanga huku mtupiaji akiwa ni Taddeo Lwanga dk 76 kwa kichwa akiwa ndani ya 18 baada ya Luis Miquissone kupiga kona.

Injinia Hersi Said ambaye anatoka katika kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga amesema kuwa kwa kilichotokea hawana cha kufanya.

“Hatuna cha kufanya kwa kuwa imeshatokea na ilikuwa fainali na kila mtu ameona kwamba ilikuwa ngumu na mwisho wa siku tumepoteza hivyo tunajipanga kwa wakati ujao.

“Wachezaji wamejitahidi na wamefanya kazi nzuri hivyo wanastahili pongezi katika hilo. Wakati ujao tutafanya vizuri,”.

SOMA NA HII  YANGA: HATUNA HOFU NA SIMBA