Home Simba SC MRITHI WA LUIS MIQUISSONE SIMBA ATUA BONGO

MRITHI WA LUIS MIQUISSONE SIMBA ATUA BONGO

 KLABU ya Simba imeunasa mkataba wa winga wa kimataifa wa Malawi, Peter Banda ambaye imefahamika kuwa mchezaji huyo amemaliza mkataba wake wa mkopo ndani ya Klabu ya Sheriff ya Moldovia.

Winga huyo anahusishwa kusajiliwa na Simba ili kuziba nafasi ya Luis Miquissone anayetajwa kuingia anga za Al Ahly ya Misri.

Nyota huyo ambaye ni mchezaji wa Big Bullets ya Malawi aliweka wazi kwamba amemaliza mkataba wake na Sherif alikokuwa kwa mkopo na kubainisha kuwa yupo kwenye kukamilisha usajili wake ndani ya Simba.

“Mkataba wangu wa mkopo ndani ya Sherif umemalizika hivyo kwa sasa ninasubiri kukamilisha dili la kujiunga na Simba ambapo tupo katika hatua nzuri za kukamilisha mazungumzo, ” amesema.

Winga huyo yupo Dar ambapo timu yake ya Big Bullets imewasili kushiriki Michuano ya Kagame na leo kitacheza dhidi ya Yanga kwa kuwa wapo kundi moja ambalo ni A.

SOMA NA HII  KISA KUANZIA SANA BENCHI..MORRISON ASHINDWA KUJIZUIA SIMBA...ATOA KAULI TATA..ADAI ATAPAMBANA...