Mwandishi wa habari Mwandamizi na Mchambuzi wa Soka la Bongo Edo Kumwembe ametoa ushauri wa bure kwa Viongozi wa klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC, katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa 2021/22.
Simba SC ipo kwenye mkakati wa kukiboresha kikosi chao katika kipindi hiki, ili kuwa na ubora wa kupambana kwenye michuano ya Ligi Kuu na ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
SOMA PIA : KIUNGO ALIYETEMWA KAGERA SUGAR AFUNGUKA KUSAINI SIMBA MIAKA MITATU
Kumwembe ametoa ushauri huo akiwa kwenye kipindi cha Sports Arena kinachorushwa na Wasafi FM, ambapo amesema kuna haja kwa viongozi wa Simba SC wajitafakari na kuacha mpango wa usajili kwa kelele za mitandaoni.
Kumwembe amesema: Simba hawajapoa…na wakifuata usajili wa mitandao watakwama…kwa mfano katika issue ya wachezaji wa kigeni Simba lazima wakate watu kisha waweke watu….zaidi ya kumuonea Chikwende, ungemkata nani mwingine?
Ukimuacha Kagere akaenda Yanga au Azam tutalaumiana mbele ya safari…nafasi iliyopo ni ya kuuzwa mtu ndipo aje mtu…kama Miquissone vile.
PIA SOMA: HAJI MANARA: SENZO ALIAJIRIWA ILI ANIFUKUZE
Local players hakuna wachezaji wa ajabu sana wa kukimbilia..foreigners waliopo Simba ni bora sana…akatwe nani sasa?. Chama? Morrison? Lwanga? Wawa? Bwalya? Miquissone? Josh?….au….tatizo mashabiki wanapenda usajili wa fasheni…
Simba SC mpaka sasa imetangaza kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka Malawi Peter Banda kwa mkataba wa miaka mitatu.