IDD Kipagwile na Paul Peter nyota wa Azam FC wana kazi ya kuendelea pale walipoishia kwa kutimiza majukumu yao watakapokuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya KMKM.
Vijana hao waliweza kutupia kwenye mechi za awali ambapo ile ya kwanza katika Kombe la Kagame dhidi ya mabingwa watetezi KCCA ya Uganda ni Peter alitupia mabao mawili yote.
Katika mchezo wa kwanza ubao wa Azam Complex ulisoma Azam FC 2-0 KCCA na ule wa pili ubao huo ulisoma Azam FC 1-0 Messager Ngozi FC bao lilipachikwa na Kipagwile.
Azam FC imekuwa ni timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Kagame hivyo ikipoteza leo ama kupata sare hakuna kitakachoharibika kwao.
Vivier Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa vijana wana kazi ya kuendelea pale ambapo waliishia.