Home Azam FC AZAM FC, KMKM ZATINGA HATUA YA NUSU FAINALI KAGAME

AZAM FC, KMKM ZATINGA HATUA YA NUSU FAINALI KAGAME


USHINDI wa mabao 3-2 dhidi ya Azam FC ambao waliupata KMKM kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Kagame unafanya timu hizo mbili zote kutinga hatua ya nusu fainali.


Azam FC kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex haikuwa na cha kupoteza kwa sababu iliweka rekodi ya kutinga hatua ya nusu fainali ikiwa na mechi moja mkononi.

Sasa katika hatua ya nusu fainali ni timu mbili kutoka Tanzania zitacheza ambapo ni Azam FC na KMKM zote kutoka katika kundi B.

Wawakilishi wengine wa Tanzania ambao walikuwa ni Yanga walifungashiwa virago jana kutoka katika kundi A ambalo walikuwepo baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Express ya Uganda.

Sasa nusu fainali ni:- Express FC vs KMKM SC.
 na Azam FC vs Nyasa Big Bullets ambapo washindi wa kila hatua watakutana hatua ya fainali.

Aliyekuwa bingwa mtetezi wa taji la Kagame, KCCA alishavuliwa ubingwa kwa kuwa kwenye kundi B ambalo alikuwepo alikusanya pointi tatu na kumaliza akiwa nafasi ya nne. 
SOMA NA HII  YANGA YAFUNGASHIWA VIRAGO KAGAME CUP, UWANJA WA MKAPA