kimataifa

LUKAKU KUIBUKIA CHELSEA

admin August 8, 2021 4:43 am


MSHAMBULIAJI Romelu Lukaku ambaye alisepa ndani ya Klabu ya  Chelsea mwaka 2014 na kwa sasa anakipiga ndani ya Inter Milan amewaambia mabosi wake kwamba wamruhusu aondoke ikiwa atapata ofa nzuri mezani.

Nyota huyo amefunga jumla ya mabao 24 na timu hiyo ya Inter Milan  ilitwaa taji la  Serie A msimu uliopita na inaelezwa kuwa Chelsea wapo mezani kufanya mazungumzo ili kumpata mchezaj wao wa zamani.

Dau ambalo wameweka mezani kwa ajili ya kupata saini yake ni pauni milioni 97.5 jambo ambalo linaonesha kwamba anaweza kuondoka hapo huku habari zikieleza kuwa tayari kila kitu kinakwenda sawa.

Kutokana na dau kuwa nono imekuwa ngumu kwa Inter Milan kugomea ishu hiyo jambo ambalo limepelekea aandaliwe mkataba wa miaka mitano baada ya kufanyiwa vipimo kwa raia huyo wa Ubelgiji ambapo awali Inter Milan walikataa ofa ya pauni milioni 80.


VIDEO: UKONDE WA YANGA ANA AMINI ATAKUWA KIKOSINI HAPO MSIMU UJAO SIMBA WABADILI GIA ANGANI..SASA KUONYESHANA UBABE NA YANGA MOROCCO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply