Yanga SC

BREAKING: AUCHO ATAMBULISHWA RASMI YANGA, AFUNGUKA

admin August 9, 2021 12:43 pm


RASMI: UONGOZI wa Yanga leo Agosti 9 umemtangaza nyota mpya Khalid Aucho, winga kutoka nchini Uganda.

Nyota huyo alishuka Tanzania usiku wa kuamkia leo kisha akamalizana na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu,  Nasreddine Nabi. 

Ni miaka miwili amesaini kwa ajili ya kuitumikia timu ya Wananchi ambayo inashiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Ligi ya Mabingwa Afrika ni michuano ya kimataifa ambayo Yanga itashiriki baada ya Tanzania kupata nafasi nne za kupeleka timu na timu hiyo ilimaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye ligi.

Aucho amesema:”Malengo ya kila mchezaji ni kucheza timu kubwa, Yanga ni timu kubwa hivyo kwa sasa mimi ni njano na kijani,” .

MANARA AENDELEA ‘KUTEMA NYONGO’ MSIMBAZI, SAFARI HII KAJA NA HILI… KABWILI ABAKI, SHIKALO NA METACHA MNATA PANGA LIMEWAKUTA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply