Simba SC

SIMBA YATHIBITISHA KUSEPA KWA CLATOUS CHAMA

admin August 13, 2021 11:43 am


UONGOZI wa Simba umeweka wazi kwamba msimu ujao hautakuwa na nyota wao Clatous Chama ambaye amepata dili la kujiunga na Klabu ya RS Berkane.

Mbali na Chama pia Luis Miquissone naye amesepa ndani ya kikosi hicho ambapo anatajwa kumalizana na Al Ahly ya Misri. 

Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga, amethibitisha asubuhi kwamba nyota wao mahiri, Clatous Chota Chama amejiunga na timu ya RS Berkane ya Morocco.

Ameongeza kuwa wao wameridhia kwa kuzingatia maslahi mapana ya mchezaji pamoja na klabu ya Simba.

Alipokuwa ndani ya Simba kwa msimu uliopita alifunga jumla ya mabao 8 na kutoa pasi 15 za mabao na alikuwa ni kinara kwa pasi za mwisho.

WEWEEH..AJIBU BADO YUPO SANA MSIMBAZI..AONGOZA NYOTA HAWA WAPYA KWENDA MOROCCO RAIS CAF AWASILI DODOMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply