Tetesi za usajili

DITRAM NCHIMBI AINGIA ANGA ZA BIASHARA UNITED, AFUNGUKA HATMA YAKE

admin August 14, 2021 11:43 am


 DITRAM Nchimbi nyota wa timu ya Yanga anatajwa kuwa kwenye rada za Biashara United ambao wanahitaji kupata saini yake.

Biashara United inashiriki Kombe la Shirikisho msimu huu na ipo kwenye mpango wa kuboresha kikosi chake.

Miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuwa kwenye hesabu za kutua hapo ni pamoja na Nchimbi ambaye msimu wa 2020/21 aliweza kutupia bao moja ilikuwa mbele ya Gwambina FC.

Kuhusu tetesi ya yeye kutakiwa kuondoka Yanga alibainisha kwamba anaziona kwenye mitandao huku yeye akitambua kwamba ni mali ya Yanga.

“Mimi nipo Yanga na nimekuwa nikiskia kwamba kuna timu ambazo zinanihitaji hilo mimi sijui. Sifikirii kuondoka Yanga kwenda timu nyingine kwa kuwa mimi ni mchezaji wa Yanga,” amesema.

AZAM FC YAZINDUA NEMBO MPYA, YAANZA KUTUMIKA RASMI VIDEO: WAFAHAMU WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply