Habari za michezo

ALLY KAMWE, AHMED ALLY WAVAANA KISA HIKI HAPA

Staff Desk December 24, 2023 3:34 pm

Ally kamwe ameijia juu Interview ya Ahmedy Ally aliyoifanya jana baada ya Simba kupata Sare dhidi ya Kmc akisema wachezaji wao hawajitumi. Kupitia Instagram Ally kamwe aliandika ujumbe huu kwa Ahmed Ally

“Shida ni kwamba .. Timu inaposhinda Msemaji unajimilikisha ushindi huo. Unatamba nao na kujipa kila aina ya majina kuonyesha kwamba Wewe ni KILA KITU kwenye Ushindi.

Lakini timu inapopata matokeo mabaya, Unajitenga nayo. Unaanza kutupa lawama hadharani kwa wachezaji kuwa hawana Ubora na Uchu wa kuipa Timu mafanikio..Huku ni KUKOSA HESHIMA.

Ni Ubinafsi na unaonyesha ni kwa kiasi gani Msemaji upo kwa ajili ya kulijenga jina lako na sio kuijenga Taasisi yako. Na hii ni mbaya pindi Interest binafsi zinapotangulia kuliko Interest za Taasisi.

Jambo moja ambalo inatupasa tuelewe, Nyakati nzuri na mbaya ni kwa ajili ya wote. Hakuna mchezaji anayekwenda uwanjani ili apoteze mchezo.

Kuwazodoa na kuwasema hadharani wachezaji wako ni kutaka kuwachonganisha na mashabiki. Ni ishara pia ya kutoheshimu kazi yao.

Na hata inapobidi, wachezaji wakatakiwa kusemwa, mwenye jukumu hilo ni Mkuu wa Benchi la Ufundi, Sio msemaji wa Timu.

HAWA HAPA MASTAA 5 SIMBA WANAOKULA ‘GOOD TIME’ BILA JASHO YANI…. KWANI MNASEMAJE… GAMONDI,BENCHIKHA NJIA TOFAUTI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply