Home Simba SC KISA CHAMA KUSEPA MSIMBAZI..MANARA ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA HAYA

KISA CHAMA KUSEPA MSIMBAZI..MANARA ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA HAYA

BAADA ya Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga kuthibitisha timu hiyo kumuuza mchezaji wake, Cloutus Chama kwa miamba ya soka ya Morocco, Berkane RBS.

Aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara amesema haya

โ€œNiliiona miguu yako siku ya kwanza nikapagawa na ufundi wako..

Nakumbuka tukiwa Kitwe Zambia,Picha hiyo ya mbele ikatawala Katika mitandao na Magazeti ya kwenu.

Nakumbuka pia wakati tunarudi ukaniambia tutafuzu kwenye mechi ya marudiano, ahhhhh Mwamba ukafunga goli maridadi mno dhidi ya Nkana.

Real friend na Jirani yangu nikutakie kheri nyingi katika maisha mapya Morocco na naamini utafanikiwa ๐Ÿ’ช๐Ÿฟ

Nani aliniamini nilipokuita Mwamba wa Lusaka August 2018?

Hakika Tanzania ilishuhudia talent murua kwa miaka mitatu na itoshe tu kusema nitakumiss sana my hero !!โ€- amesema aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara.

SOMA NA HII  SHABIKI SIMBA:- ILI KESHO TUSHINDE....WACHEZAJI WAPEWE iPhone 15 na MIL 100 KILA MMOJA...