Mabingwa wa Soka Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC) Simba SC, wametangaza kumsajili kiungo kutoka Senegal Pape Ousmane Sakho.
Kiungo huyo mwenye umri wa miama 24 amethibitishwa Msimbazi, akitokea klabu ya Teungueth ya nchini kwao.
Msimu uliopita Pape alitangazwa kuwa mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya soka nchini Senegal, jambo ambalo linatajwa kunogesha usajili wake ndani ya Simba SC.
Hata hivyo inaaminika kuwa Pappe ndiye anatajwa kuwa mbadala wa moja kwa moja wa Luis Jose Miquissone ambaye anajiunga na Al Ahly ya Misri.
Pappe ambaye anatoka nchi moja na star wa Liverpool , Sadio Mane kitu ambacho ni sawa na kusema ni mdogo wake kwa kuwa owte ni raia wa Senegal, anatajwa kuwa na kasi na uwezo kama wa Luis Miquissone