Simba SC

BREAKING:SIMBA YAMTANGAZA MCONGO MPYA, YEYE NI BEKI

admin August 15, 2021 12:43 pm


 KIKOSI cha Simba leo kimemtambulisha nyota mpya ambaye ni beki kutoka nchini Congo.

Ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Congo DR na beki kisiki, Henock Inonga Baka (26) ambaye kwa sasa ni mali ya Simba.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, Simba wameandika kwamba nyota huyo kwa sasa ni mali halali ya Simba.

Anakuwa nyota wa nne wa kigeni kutambulishwa Simba ambapo wa kwanza alikuwa ni Peter Banda raia wa Msumbiji kisha Duncan Nyoni na Pape Sokhu raia wa Senegal.

Timu hiyo imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2021/22 ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

AZAM FC KUWEKA KAMBI ZAMBIA VIDEO: KUMBE JEMBE ALIKATAZWA KUWA MWANDISHI, SABABU YA JINA YAWEKWA WAZI, ANACHANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply